Cheka Tu wakiwa na Maua Sama usiku wa leo wanafanya moja kati tukio kubwa la burudani katika maeneo ya Warehouse Masaki jijini Dar es Salaam.
Leo msanii Maua Sama atazindua EP yake wakati Cheka Tu wenyewe watatoa burudani za viwango vya juu katika suala zima la uchekeshaji wakipewa ngumu na Leonbet ambayo ni Kampuni mpya ya Ubashiri Tanzania.
Coy Mzungu ambaye ndio Kiongozi wa Cheka Tu ameeleza namna ambavyo Show hiyo imeandaliwa kwa ukubwa wa viwango vya juu hususani baada ya Leonbet kampuni kutokea Malta kuweka pesa nyingi za kufanikisha hilo.
”Sanaa imekuwa sehemu ya kutoa ajira lakini haiwezi kutoa ajira pekee yake lazima ipate wadau wengine ambao wanaiwezesha hiyo sanaa kutoa ajira kwa ukubwa zaidi hilo linawezekana kwa Makampuni Makubwa kama Leonbet kushiriki kutoa ajira”>>> Coy
Kwa upande wa Jerome Duforg ambaye ni Mkurugenzi wa Leonbet Afrika ameeleza namna ambavyo wameamua kuingia Tanzania kwa miguu miwili.
”Leonbet imeanzishwa 2008 nchini Malta na sasa ipo katika nchi 20 duniani tukianzia mwaka jana Uongozi uliamua kuingia Afrika na baada ya utafiti tukaona kuna nafasi nzuri ya kufanya biashara hapa kwa sababu mna miundombinu, internet yake ina kasi na watu wake wana akili”>>> Jerome Dofourg