Klabu ya soka ya Chelsea January 3 ilivunja mwiko wa kutopata matokeo mazuri kwa kuiadhibu klabu ya Crystal Palace kwa jumla ya goli 3-0 katika uwanja wa ugenini. Chelsea ambayo ilikuwa katika wakati mgumu kwa kupoteza mechi nyingi kuliko kawaida yake, wachezaji wameanza kuwa na furaha na matokeo hayo.
Nahodha wa klabu hiyo John Terry amefunguka na kuanza kujivuna kuwa hiyo ndio Chelse ya mwaka uliopita imeanza kurudi, wakati Pedro na Fabregas wameonesha matabasamu yao katika mitandao ya kijamii. Terry anaamini wameanza kurejea katika hali yao ya kawaida kama ambavyo alisema Guus Hiddink kocha wa muda wa Chelsea.
“Hii sasa naweza sema ni kama Chelsea ya msimu uliopita imeanza kurudi, michezo ndio tunaipa kipaumbele lakini sifikirii kama huu ndio mwisho wa kupata matokeo mazuri. Mwaka mpya, tumeanza vizuri na tunalazimka kuendelea na ushindi kwa kila mechi. Kocha mpya amaekuja na inaonekana ameanza kuimarisha kiwango cha kila mmoja kama ilivyokuwa awali” >>> John Terry
Kufutia kupatikana kwa ushindi huo na Chelsea kupata kocha wao mpya wa muda kumeanza kuleta amani kwa wachezaji hao, hata Cesc Fabregas ambaye kuna wakati alishambuliwa na mashabiki wa Chelsea kuwa anacheza chini ya kiwango sana na Pedro Rodriguez wameanza kufurahia na kupiga self.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.