Baada ya weekend ya August 13 na August 14 kuchezwa kwa jumla ya michezo 9 ya round ya kwanza ya Ligi Kuu England kuchezwa, usiku wa August 15 ilikuwa ni zamu ya klabu ya Chelsea chini ya kocha wao mpya Antonio Conte kuwakaribisha West Ham United katika uwanja wa Stamford Bridge.
Katika mchezo huo ambao wengi walikuwa wanamsubiria Antonio Conte kuona atafanya nini baada ya makocha wapya wenzake kama Jose Mourinho wa Man United na Pep Guardiola wa Man City kuibuka na ushindi katika michezo yao ya mwanzo wa msimu wa EPL.
Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, Chelsea walianza kupata goli dakika ya 47 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Eden Hazard ila James Collins alifanikiwa kuisawazishia West Ham dakika ya 77, uhakika wa Chelsea kuondoka na point tatu ulikamilika dakika ya 89 baada ya Diego Costa kupachika goli la ushindi.