Bado klabu ya Chelsea ya Uingereza inaongozwa na kocha wake wa muda Guus Hiddink ambaye ataiongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu, Hiddink alijiunga na Chelsea kuchukua nafasi ya Jose Mourinho ambaye alifukuzwa na timu hiyo.
March 3 gazeti la Stadio Corriere dello Sport linaripoti kuwa mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich ameshawajulisha viongozi wote wa Chelsea ikiwemo benchi la ufundi kuwa Antonio Conte ndio atajiunga na Chelsea na kuwa kocha mpya wa timu hiyo, kwa mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya euro milioni 6 kwa mwaka.
Kama taarifa za Antonio Conte ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Italia atajiunga kweli na Chelsea, atakuwa kocha wa tano wa kiitaliano kuifundisha timu hiyo, baada ya Gianluca Vialla, Roberto Di Matteo, Carlo Ancelotti na Claudio Ranieri.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE