Chelsea na Arsenal ni miongoni mwa timu nyingi barani Ulaya zinazofikiria kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig Benjamin Šeško, kulingana na TEAMtalk.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anaripotiwa kutambuliwa na The Blues kama mbadala wa nyota wa Napoli Victor Osimhen, huku uongozi wa Stamford Bridge ukitaka kuimarisha safu yao ya mbele wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.
The Gunners pia wanasemekana kuwa kwenye kinyang’anyiro hicho, na inaaminika kuwa mkutano unapangwa hivi karibuni kujadili makubaliano na klabu hiyo ya Bundesliga kuhusu uwezekano wa kuhama.
Šeško ni mojawapo ya majina kwenye orodha fupi ya meneja Mikel Arteta, huku Gabriel Jesus na Eddie Nketiah wakihusishwa na kuondoka kwenye Uwanja wa Emirates. Pia wanaripotiwa kufikiria fowadi wa Bologna Joshua Zirkzee kama chaguo.
Šeško, ambaye alifunga katika mechi yake ya sita mfululizo katika sare ya 1-1 ya Bundesliga Jumamosi dhidi ya Werder Bremen, ana kandarasi kwenye Red Bull Arena hadi msimu wa joto wa 2028, lakini kifungu cha kutolewa kwenye mkataba wake kinamruhusu kusajiliwa kwa Euro milioni 65.