Chelsea na Napoli wameripotiwa kukutana mchana wa leo (Jumatano) ili kujadili kuhusu dili ambalo litamfanya Victor Osimhen kuhamia Stamford Bridge.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria aliwasilisha ombi la kutaka kuhama kwa timu hiyo ya Serie A wiki iliyopita, huku kukiwa na uhakika kwamba atapata njia ya kuondoka Italia msimu huu wa joto.
Baada ya kuvunjika kwa dili la pauni milioni 35 ambalo lingemfanya Samu Omorodion kuwasili Stamford Bridge wiki hii, The Blues bado wanawinda straika msimu huu licha ya kuhusishwa na mchezaji wa zamani wa mkopo Joao Felix ambaye amekuwa akitajwa kurejea Magharibi.
John Obi Mikel na Didier Drogba wamewasiliana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ili ajiunge na Chelsea, huku Mikel akidai: “Hatuhitaji mtu ambaye ataingia kutengeneza nafasi. . Tunataka mtu anayeweza kumaliza, kufunga mabao, na kugusa mipira.
“Mtu kama Erling Haaland. Hilo ni jambo ambalo Victor Osimhen ataleta Chelsea. Natumai kwamba mashabiki wa Chelsea hatimaye watamwona akija kwenye klabu.
Nitahakikisha namtumia ujumbe huo wa maandishi na kupiga simu, kuhakikisha Chelsea ni kipaumbele chake. !”