Chelsea inajiandaa kuongeza hamu ya kumnunua mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, kwa mujibu wa Evening Standard.
The Blues wanataka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Ijumaa, ingawa hawataweza kufikia ofa iliyoripotiwa ya mshahara iliyopendekezwa na klabu ya Saudi Pro League Al Ahli ya pauni milioni 16 kwa mwaka. Brentford wako tayari kuachana na Toney iwapo watapokea ofa ya karibu £40m.
Mshambulizi anasalia kuwa kipaumbele kwa Enzo Maresca, na pia anavutiwa na mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, anasema Gianluca Di Marzio. Chelsea wanatarajiwa kutoa ofa yao ya kwanza rasmi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 25 katika siku zijazo, huku kukiwa na matarajio ya ushindani kutoka kwa Paris Saint-Germain.
Kama ilivyo kwa Toney, Al Ahli pia wanaripotiwa kuwania Osimhen, wakiwa tayari wametoa ofa yenye thamani ya €70m kwa Napoli.