Gazeti la The Mirror linaripoti kwamba klabu hiyo inaweza kumwachilia mshambuliaji mwingine, Armando Broja, kuondoka huku Wolves wakimtaka.
“Mshambulizi wa Aston Villa Jhon Duran amekerwa na kukosa muda wa kucheza chini ya Unai Emery na sasa ametoa nukuu za kuvutia kwa vyombo vya habari vya Colombia,” gazeti hilo linaripoti.
“Duran alijiunga na Villa mwaka mmoja uliopita kutoka Chicago Fire na amekuwa nyuma ya Ollie Watkins tangu wakati huo.
“Chelsea wana nia ya kusajili mshambuliaji mpya mwezi huu na kuwasili kwa mpinzani kunaweza kumfanya Broja kuhamia kwingine kutafuta muda wa kucheza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akilengwa na Napoli na Milan. Ana mabao mawili katika mechi 17 msimu huu, lakini Christopher Nkunku akiwa ameumia tena na Nicolas Jackson kwenye AFCON, anapaswa kuwa na nafasi zaidi.”