Conte amekaa nje msimu huu baada ya kuondoka Tottenham karibu miezi 12 iliyopita ila kulingana na La Repubblica inasema Conte anaweza kurejea Premier League na Chelsea.
Miamba hao wa London tayari wamempa Conte mkataba mnono kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino msimu huu wa joto.
AC Milan na Napoli bado zipo kwenye picha, lakini hazionekani kumshinikiza Conte kwa sasa.
Conte alikuwa kocha wa Chelsea kati ya 2016 na 2018. Alishinda Ligi ya Premia katika msimu wake wa kwanza.
Pochettino ana mkataba na Chelsea hadi msimu wa joto wa 2025 na chaguo la mwaka mwingine.