Chelsea imemsajili mshambuliaji wa England anayechezea timu ya chini ya umri wa miaka wa 21 Cole Palmer kutoka Manchester City kwa dau la £40m.
Mkataba huo unajumuisha nyongeza ya pauni milioni 2.5 na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amesaini mkataba wa miaka saba na chaguo la mwaka mmoja zaidi.
Palmer alikuwa sehemu ya timu ya Uingereza ambayo ilishinda Ubingwa wa Yuropa wa Vijana chini ya miaka 21 mapema msimu huu na ni anatoka katika timu ya vijana chipukizi ya akademi ya City.
“Nimefurahi kuanza na ninahisi vizuri kusaini,” alisema. “Nimejiunga na Chelsea kwa sababu mradi wa hapa ni mzuri na kwa sababu ya jtimu yenyewe ni kubwa nitalazimika kujaribu kuonyesha vipaji vyangu.
“Ni kikosi cha vijana na chenye njaa na, tunatumai, tunaweza kufanya kitu maalum.” Palmer alifunga bao katika mechi dhidi ya City katika kombe la Charity shield , mbali na goli alilofunga katika mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Sevilla
Meneja wa City Pep Guardiola hapo awali alisema kwamba Palmer hataruhusiwa kuondoka kwa mkopo.