Weekend ya Jumamosi ya January 30 na Jumapili ya January 31 Ligi Kuu Uingereza haukuchezwa mchezo wowote wa Ligi Kuu, ila kulikuwa na michezo ya Kombe la FA, Jumapili ya January 31 ilichezwa michezo miwili ya Kombe la FA, mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Carlisle United dhidi ya Everton na kumalizika kwa Everton kuibuka na ushindi wa goli 3-0.
Baada ya hapo klabu ya Chelsea ambayo inafundishwa na kocha wake wa muda Guus Hiddink ilikuwa ugenini kucheza na klabu ya Milton Keynes Dons inayoshiriki michuano ya Championship, Chelsea ambayo msimu huu imekuwa ikisuasua katika michezo yake ya Ligi Kuu, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-1.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Oscer ambaye amefunga hat-trick, Oscer alifunga goli la kwanza dakika ya 16 na dakika ya 32 na 44 alifunga magoli mengine mawili, baada ya Milton Keynes Dons kupata goli la kusawazisha dakika ya 22 kupitia kwa Darren Potter, kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard alipachika goli la nne dakika ya 55 na Bertrand Traore alihitimisha goli la tano dakika ya 62.
Video ya magoli ya mchezo wa Milton Keynes Dons Vs Chelsea
https://youtu.be/FEzuzhFAwjQ
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.