Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema kitendo cha Marekani kujitoa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ni pigo kubwa, Spahn ameandika kwenye ukurasa wa Twitter kuwa kujitoa kwa Marekani kutoka WHO ni pigo kubwa kwa ushirikiano wa Kimataifa, na kutoa wito wa ushirikiano zaidi kupambana na majanga.
Waziri huyo ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya utapendekeza mageuzi kuifanya WHO kuwa imara zaidi.
China pia imeikosoa Marekani kwa kujitoa kutoka shirika hilo na kusema hatua hiyo itakuwa na athari mbya kwa Mataifa yanayoendelea.
Marekani imemfahamisha rasmi jana Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusiana na Nchi hiyo kujitoa WHO kwa madai Shirika hilo limeshindwa kupambana na corona na linaipendelea China.
KWA MARA YA KWANZA ANDENGENYE AZUNGUMZA KIGOMA ”RUSHWA NI ADUI SIJAWAHI KUINGIA KWENYE JAMBO HILO”