China inatarajiwa kutengeneza treni mpya ya kisasa inayoelea (Floating Train) yenye kasi kubwa zaidi duniani ya 600mph inayosafiri kwa kasi kuliko ndege ambayo inatarajiwa kuunganisha Miji yote ya Nchi hiyo na kuchagiza mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri duniani.
Wasanifu wa mradi huo mkubwa wa China tayari wameanza kuijaribu treni hiyo ya T-Flight ambayo husafiri katika mfumo uliotengenezwa kama mabomba au mirija iliyoundwa kupunguza shinikizo la hewa na kuisukuma mbele treni hiyo kupitia teknolojia ya “hyperloop” bila matairi.
Hiyo ndio sababu kuu ya kuitwa treni inayoelea, Mradi huo tayari umeweka rekodi ya dunia kwa kasi ya 400mph kwa saa kupitia treni ya kisasa ya abiria ya Shaghai Maglev inayosafiri kwa kasi zaidi duniani, ujio wa T-Flight unatarajiwa kuvunja rekodi hiyo na kusafiri kwa kasi zaidi ya 621mph.
China haiko peke yake katika kufanya majaribio kwa kutumia teknolojia ya “hyperloop”, Nchi nyingine kama vile Uswizi, Uholanzi, Marekani na Canada zimeanzisha miradi ya aina hiyo huku India ikitangaza nia kwa kusema kuwa utafiti wake kuhusu teknolojia hiyo utaanza rasmi 2026.