China imetangaza kuwa itafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Jeshi la Urusi mwezi huu, katika jitihada za kuimarisha ushirikiano wa Kijeshi na Kiuchumi kati ya Washirika hao wawili wanaopinga kile wanachokiona kama utawala wa Marekani katika masuala ya Dunia.
Wizara ya Ulinzi ya China imesema majeshi ya anga na majini yatashiriki katika mazoezi hayo yanayoitwa North-Joint 2024, yatakayofanyika angani na katika Bahari ya Japani na Bahari ya Okhotsk.
Mazoezi hayo yanalenga kuongeza ushirikiano wa kimkakati kati ya Majeshi ya China na Urusi, na pia kuboresha uwezo wa kukabiliana na vitisho vya kiusalama.
Pande zote mbili zitatuma Meli za kivita kufanya doria za pamoja katika maeneo husika ya Bahari ya Pasifiki, huku China pia ikishiriki katika mazoezi makubwa ya Urusi yajulikanayo kama Ocean-2024.
Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi ya China haijatoa tarehe kamili ya kuanza kwa mazoezi hayo.