Serikali Ya Jamuhuri Ya Watu Wa China Imetoa Msaada Wa Magari 8 Yenye Thamani Dola Laki Nne Ambazo ni Sawa na Zaidi ya Milioni Mia Tisa na Thelathini Kwa Fedha za Tanzania, pamoja na kuleta wataalam wa kutoa mafunzo Kwa madereva wa jumuiya hiyo Kwa lengo la kuboresha shughuli za EAC.
Akiongea mara baada ya kukabidhi magari hayo yaliyokabidhiwa makao makuu ya jumuiya ya Afrika mashariki EAC jijini Arusha.
Balozi wa china CHEN MINJUAN amesema Serikali ya watu wa China imekuwa ikishirikiana na umoja wa jumuiya ya Afrika mashariki katika masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na kusaidia kukuza demokrasia na uwajibikaji wa utawala Bora.
Akizungumza Kwa niaba ya Katibu Mkuu EAC Mkurugenzi wa sekta ya Maendeleo ya jamii Irene Isaka amesema magari hayo yataenda kuwasaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo matamasha ya vijana na wajasiriamali kwenye mataifa 7.