Kwa mujibu wa tovuti ya USA today J Hotel Shanghai Tower, ndio jengo la pili (2) kwa urefu zaidi duniani likiwa mara mbili ya mnara wa Eiffel ulioko katika jiji la paris nchini Ufaransa
Hoteli hiyo ilifunguliwa rasmi Juni 19 mwaka huu, ikiwa na urefu wa futi 2,000 kwenda juu
Kulala kwenye hoteli hiyo kwa usiku mmoja ni zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 1.2 kwa chumba cha kawaida, huku gharama ikizidi kupanda na kufikia shilingi milioni 24.2 kwa chumba chenye hadhi ya juu zaidi yaani Presidential Suite.
Pia Hotel hiyo yenye vyumba 165 ina huduma za kisasa na viwango Lift inayopanda na kushukua ambapo speed yake ni mita 18 kwa sekunde (18m/sec), migahawa 7 tofauti, Swimming pool N.k.
Licha ya jengo hilo kuwa refu zaidi lakini rekodi inashikiliwa na hoteli kutoka Dubai Gevora iliyotunukiwa na kutambuliwa na tuzo ya Guinness Book of Records.