China siku ya Jumanne ilizitaka Marekani na Uingereza kuacha kuingiza siasa katika suala la usalama wa mtandao, kuikashifu China na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya upande mmoja.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema, “Ni ujanja wa kisiasa kwa Marekani na Uingereza kurekebisha upya kile kinachoitwa mashambulizi ya mtandaoni yaliyofanywa na China na kuwawekea vikwazo watu na mashirika ya China,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
“China haijaridhishwa vikali na hili na inapinga vikali,” alisema.
Maafisa wa Marekani na Uingereza siku ya Jumatatu walifungua mashtaka, kuweka vikwazo, na kuishutumu Beijing kwa kampeni kubwa ya ujasusi mtandaoni ambayo inadaiwa kuwakumba mamilioni ya watu wakiwemo wabunge, wasomi na waandishi wa habari, na makampuni yakiwemo wanakandarasi wa ulinzi.
Mamlaka katika pande zote za Atlantiki walilipa jina la utani kundi la udukuzi Advanced Persistent Threat 31 au “APT31,” na kuliita tawi la Wizara ya Usalama wa Nchi ya China.
Maafisa waliondoa orodha ya watu wanaolengwa: wafanyikazi wa Ikulu ya White House, maseneta wa Marekani, wabunge wa Uingereza, na maafisa wa serikali kote ulimwenguni ambao waliikosoa Beijing.