China imekataa kuungana na tamko la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) la kulaani mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini Myanmar.
Jumatatu ya wiki hii serikali ya Myanmar (zamani iliitwa Burma), ilipinduliwa na jeshi. Kiongozi wa chama tawala cha nchi hiyo, Aung San Suu Kyi na wanasiasa wengine, wanashikiliwa na jeshi hilo.
Mapinduzi hayo yamesababisha kuibuka kwa maandamano katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Yangon, kupinga mapinduzi hayo.
Kutokana na mapinduzi hayo, Baraza la Usalama la UN ambalo China ni moja wa wanachama wake, lilikutana Jumanne wiki hii kutoa tamko la pamoja la kulaani mapinduzi hayo. Hata hivyo, China imekataa kuunga mkono tamko hilo.