China imefanikiwa kurusha satelaiti mbili mpya za Mfumo wa Satellite wa Uongozaji wa BeiDou-3 (BDS-3) angani kwenye Kituo cha Kurushia Satelaiti cha Xichang kilichoko kusini-magharibi mwa Mkoa wa Sichuan.
Satelaiti hizo mbili, ya 57 na 58 za mfumo wa BeiDou, zilirushwa jana saa 5:26 asubuhi kwa roketi ya kubebea ya Long March-3B na Yuanzheng-1 iliyounganishwa na roketi ya kubeba.
Hizi ni setilaiti za kwanza za obiti ya kati ya Dunia (MEO) kurushwa tangu BDS-3 ilipoidhinishwa rasmi kutoa huduma za uongozaji za satelaiti duniani kote. Baada ya kuingia kwenye obiti na kukamilisha majaribio ya obiti, zitaunganishwa kwenye mfumo wa BeiDou.
Zikilinganishwa na satelaiti za awali za MEO za mfumo wa BeiDou, satelaiti hizi mpya zimeboresha ufanyaji kazi wake na utendaji katika maeneo mbalimbali. Zitaboresha uaminifu na uwezo wa huduma wa mfumo wa BeiDou. Pia zitaweka msingi wa utengenezaji wa satelaiti za BDS za kizazi kijacho.