Kuna taarifa zinazowahusu Raia wa nchi ya China wanapokua Tanzania baadhi yao huonekana wakiwa wanaishi kwenye makazi ya kawaida huamua kutengeneza viwanda vyao,kitu ambacho kimeonekana kuwa kero kwa raia wanaoishi maeneo hayo.
John Haule ambaye ni Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje amekubali kulizungumzia hili>>’Kuna mwandishi mmoja aliwahi kutoa kero kwa baadhi ya ndugu zetu wachina walioko nchini ambao wameanzisha viwanda kwenye makazi bila vibali,sasa hili ukiangalia sio tatizo lao kwakweli sisi tunazo mamlaka,mamlaka zetu ndizo zinazotakiwa kutusaidia’
‘Kwanza kusajili biashara zote zinazofanyika hapa nchini kusajili viwanda vyote vinavyofunguliwa hapa nchini na hakuna mtu atakayesema hawa walioanzisha kwenye makazi hawaonekani,wanaonekana na mamlaka zipo halmashauri zetu,manispaa zetu zipo na wana viongozi kama kweli wapo mi nafikiri baada ya taarifa zao kufikishwa kwao wawatembelee wawaone kama kweli hawana leseni kama kweli wameanzisha viwanda kwenye maeneo yasiyoruhusiwa na hatua zichukuliwe’
‘Hatua mojawapo kwanza ni kuwaelimisha kuwa viwanda kama hivyo inabidi vianzishwe kwenye maeneo gani lakini pili kuwaonyesha maeneo hayo na kuwapa vibali vya ujenzi badala kuonekana kama ni tatizo ambalo haliweze kutatuliwa,naamini sio tatizo kubwa maana tunalimudu pia,ukiona dalili ya kiwanda ripoti maeneo husika naamini hatua zitachukuliwa’.