Tatizo kubwa kwa vijana wanaomaliza elimu ya Juu TZ ni ajira.. lakini ni nchi nyingi zina tatizo kama hilo, Utafiti wa China unaonesha Mwaka huu pekeake vijana wanaomaliza Vyuoni na kuingia kusaka ajira wako kama watu Mil.7.49.
Utafiti huo umeonesha hali ilikuwa hivi mwaka jana waliomaliza Vyuoni na kupata ajira, mishahara yao ilikuwa hivi;
No.1: Game designers: Ni kama utani hivi lakini ndio ukweli wenyewe, katika soko la ajira China watu walioongoza kwa kulipwa vizuri ni watu wanaotengeneza game hizihizi kama Playstation hivi, au Nintendo.. wao walilipwa kama Dola 844 (Ths. 1,870,000/=) kwa mwezi.
No.2: Website Designers na Internet Developers: Kiukweli China ni moja ya Nchi ambazo zinakuja juu kwa masuala ya Technolojia.. Kwao Mtaalam wa masuala ya Website na IT alilipwa kama Dola 834 (Tshs. 1,850,000/=)
No.3: Computer Software Engineers: Kama umesomea masuala ya kutengeneza software za computer uko kwenye nafasi nzuri mtu wangu, China malipo ya mtu mwenye kazi hiyo kwa mwezi ni Dola 820 (Tsh. 1,820,000/=) kwa mwezi.
No.4: Managers na Supervisors: Nafasi ya Meneja au Msimamizi Mkuu wa mradi alilipwa Dola 787 (Tshs. 1,750,000/=)
No.5: Loan Officers: Afisa Mikopo ndani ya China mshahara wake ni Dola 786 (Tshs. 1,745,000/=)
No.6: Architects: Hapa wanaoguswa ni wale Engineers wa masuala kama ya Ujenzi na Wataalam wa Mipango miji. Malipo yao ilikuwa Dola 769 (Tshs. 1,708,000/=)
No.7: Sales Managers: China kama aliyeingia kwenye Soko la ajira na amesomea masuala ya Kusimamia Mauzo basi kwenye Top Ten ajira yake nayo ipo. Mshahara wake ni Dola 761 (Tshs. 1,690,000/=)
No.8: Marketing Manager: China wanazalisha bidhaa nyingi sana ambazo zinaingia kwenye Soko la Dunia, kumbe kuna uhitaji pia Wataalamu wa kuzisogeza bidhaa hizo Sokoni na kuhakikisha zinanunulika. Meneja Masoko China alilipwa Dola 759 (Tshs. 1,690,000/=)
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.