Tumesikia mara nyingi tangu kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, nchi za Ulaya na Marekani zikitoa misaada ya kukabiliana na ugonjwa huo, leo China nayo inakuwa moja ya nchi zilizoweka nguvu kwenye jitihada za kusaidia kukabiliana na Ebola.
China imeingiza msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na madawa, vifaa tiba na wataalamu.
Vifaa hivyo vimewasili uwanja wa ndege nchini Ghana na vinatarijwa kusambazwa Guinea, Liberia na Sierra Leone ndani ya siku chache baada ya kuwasili.
Chanjo dhidi ya Ebola inatarajiwa kuanza kusambazwa muda wowote japo baadhi ya wataalamu wamedai chanjo hiyo haitosaidia wale ambao tayari wana maambukizi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook