China iliweka sera ambayo iliwazuia watu kuzaa watoto zaidi ya mtoto mmoja, baada ya kufanya utafiti wakagundua kwamba watu wazima ni wengi zaidi kuliko watoto na vijana kwenye nchi hiyo, hii ilimaanisha kuna kizazi ambacho kingekuwa na uhaba wa watu, hasa wale ambao ni watoto sasa hivi wakifikia hatua kuwa watu wazima.
Baada ya majibu wa utafiti huo, waliamua kulegeza utaratibu ambapo watu ambao wana mtoto mmoja waliruhusiwa kuongeza mtoto mmoja tu hivyo mwisho ni kila familia inatakiwa kuwa na watoto wawili tu!
Mwaka huu peke yake China inatarajia ugeni mkubwa wa watoto zaidi ya milioni moja kuzaliwa.
Miaka ya 1970 walipitisha utaratibu wa kila familia moja kuwa na mtoto mmoja kwa mjini na wale wa kijijini waliruhusiwa kuwa na watoto wawili tu iwapo wa kwanza akizaliwa wa kike.
Mpaka mwisho wa mwaka 2014 kulikuwa na wanawake zaidi ya milioni moja wajawazito ambao wanatarajia kujifungua ndani ya 2015.
Sensa ya 2010 ilionesha China ina jumla ya watu bilioni 1.35, ikifuatiwa na India bilioni 1.25 huku Marekani ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na watu milioni 316.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook