Siku ya leo msanii Chinno ametangaza kurejea nyumbani kwao Ifakara Morogoro ambapo atarejea maalum kwaajili ya uzinduzi EP yake ambayo ameipa jina la Sumu ambayo itakua na jumla ya nyimbo sita pamoja na bonus track
Chinno amesema hatoenda peke ake Morogoro anatarajia uwepo wa wasanii wakubwa ambao ni kaka zake akiwemo Marioo kwenda kumsupport kwani tayari amewaalika.
Chinno ameongezea akisema jina la Ep sumu halina maana kama ambayo wengi wanafikiria kuwa ni kutokana na zile tetesi ambazo msanii mwenzake Marioo alisema kuwa anahisi Chinno amehusika kwenye kumuwekea sumu na kusema kuwa kwa upande wake kila kitu kuhusu yeye na Marioo wako sawa.