Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja habari zilizoandikwa ni hii habari kwenye gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari ‘Aina tano za vyakula hatari’
#MTANZANIA Wataalam waainisha aina 5 vyakula hatari, nyama ya nundu ya ngo'mbe, ngozi ya kuku, clips, bisi, chipsi pic.twitter.com/6od6UiPH7b
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa afya za wananchi mbalimbali zipo hatarini, kutokana na ulaji wa vyakula mbalimbali ambavyo ni hatari kiafya. Wataalamu wa chakula na lishe wameainisha aina tano za vyakula ambavyo ni hatari katika mwili wa mwanadamu, vikitajwa kusababisha maradhi mbalimbali.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, walaji wa nyama ya nundu ya ng’ombe, ngozi ya kuku, clips na bisi wapo katika hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza, ikiwamo shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo.
Taarifa hiyo inakuja siku mbili, baada ya mtaalamu wa lishe ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ulumbi Kilimba kulieleza gazeti la Mtanzania kuhusu athari za ulaji wa chips.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Lishe wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Julieth Shine, alisema si chips pekee ambazo ni hatari bali vyakula ambavyo hukaangwa kwa kutumbukizwa kwenye mafuta ni hatari kiafya.
Source: Gazeti la Mtanzania
Unaweza kuzipitia habari nyingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania
#MWANANCHI Vyama tisa vya siasa vipo hatarini kufutwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo na matakwa ya kisheria pic.twitter.com/81OATgHUw4
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#NIPASHE Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Mpinga amepiga marufuku polisi jamii kufanya kazi za polisi pic.twitter.com/LspxPECNGP
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#NIPASHE Lissu aliyekamatwa juzi Singida asafirishwa chini ya ulinzi wa polisi kwa saa 23 mpaka kituo cha polisi Dar pic.twitter.com/Xj0EayLGo6
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#NIPASHE Watumishi wote TRA waagizwa kuwasilisha vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi kwa ajili ya uhakiki pic.twitter.com/Ngi6plFhLz
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#NIPASHE Idadi ya wagonjwa wa upasuaji MOI imeongezeka kutoka wagonjwa 20 mpaka 40 kwa siku pic.twitter.com/NAN20D2dYc
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#MTANZANIA Waziri Mbarawa asimamisha kazi wawili ATCL kwa kuteua watu wasio na sifa kwenda mafunzo ya urubani Canada pic.twitter.com/JlbKNUd30a
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#MTANZANIA Fisi, mbweha wazagaa baadhi ya maeneo Ilemela Mwanza, waingia makazi ya watu, washambulia mbuzi, mashamba pic.twitter.com/IjEWuw7ZAQ
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#JamboLEO Posho ya watumishi watakaohusika kuhamia Dom itakuwa ya siku 14, kiwango cha chini 80,000, cha juu 120,000 pic.twitter.com/HF3gcGjb2z
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#JamboLEO Madereva wazembe kutupwa mahabusu kabla ya mahakamani na kulipa faini badala ya mtindo wa sasa wa faini tu pic.twitter.com/GiAHVYNwqG
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#JamboLEO Mwanaume ambaye hajafahamika jina amekufa baada ya kudandia treni na kujibamiza maeneo ya kamata Ilala DSM pic.twitter.com/Iy77J2wgCC
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#JamboLEO Mahakama Dar imewatoza faini 50,000 wanawake wawili kwa kufungua baa muda uliopigwa marufuku na serikali pic.twitter.com/HKHg32BoOo
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#JamboLEO TRL kuongeza mabehewa 20 treni mpya ya DSM Stesheni hadi Pugu, baada ya 10 ya sasa kutokidhi mahitaji pic.twitter.com/phQZCh6Pht
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#JamboLEO Bomoabomoa kuanza nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya reli na barabara kuu zote nchini pic.twitter.com/o4QLd5m5aC
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI AUGUST 05 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI