Ripoti kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu ni kama hazisikiki sana sasahivi kutokana na jinsi ambavyo Siasa imeteka Headlines za Vyombo vya Habari, lakini taarifa ikufikie kwamba Ugonjwa huo bado upo Dar es Salaam.. wapo wanaoendelea kufariki, wapo wanaopata maambukizi na wapo pia waliolazwa na wanaendelea kutibiwa Hospitali.
Leo October 12 2015 ninayo Ripoti ya kingine kinachoendelea katika Manispaa ya Kinondoni kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu… Hii imetolewa na Afisa Afya wa Manispaa, Mathias Kapizo >>>>”Mpaka sasahivi tuna wagonjwa wapya 35… Wagonjwa 35 katika Wilaya kama Kinondoni ni watu wengi… Sehemu kubwa zilizoathiriwa na Kipindupindu kwa sasa ni Manzese, Tandale, Mabibo, Makurumla, Mburahati, Kigogo, Mwananyamala, Magomeni Sinza, Makumbusho na Kijitonyama.”
“Bahati mbaya tumepoteza watu 12 mpaka sasa kwa ugonjwa wa Kipindupindu… Kwa mujibu wa taarifa ya tarehe 12 jumla ya wagonjwa wote waliougua kipindupindu tangu kilipoanza tarehe 15 mwezi wa nane wanafikia 1564 kwa sasa…“- Mathias Kapizo.
Kuhusu idadi ya Wagonjwa waliolazwa mpaka sasa, Mathias Kapizo ameitaja hii >>>> “Kwa takwimu za leo katika wodi ya Makurumla tulikuwa na mgonjwa mmoja… Ubungo wagonjwa wawili, Mwananyamala wagonjwa watatu, Magomeni mgonjwa mmoja, Kawe wagonjwa wawili, Manzese wagonjwa watano, Tandale wagonjwa wawili, Sinza wagonjwa watano, Makongo mgonjwa mmoja, Mburahati wagonjwa sita, Kigogo wagonjwa wawili, Mbezi mgonjwa mmoja, kutoka Mlandizi wamekuja wagonjwa wawili, Wazo (Tegeta) mgonjwa mmoja, Makuburi mgonjwa mmoja, Kimara mgonjwa mmoja, Mabibo mgonjwa mmoja na Tabata mgonjwa mmoja.” >>>> Mathias Kapizo, Afisa Afya Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.
Ishu ya mlipuko wa Kipindupindu ilianza kuchukua headlines tangu asubuhi ya August 18 2015 katika Mitandao pamoja na Vyombo vya Habari TZ.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.