Winga wa Kimataiga wa Ghana aliyekuwa anacheza Hatayspor ya Uturuki Christian Atsu mwili wake umepatikana katika kifusi akiwa amefariki kufuatia tetemeki lilotokea nchini Uturuki.
Atsu alikuwa anatafutwa na timu ya uokoaji kwa muda mrefu na baadae kudaiwa amepatikana kabla ya wakala wake Murat Uzunmehmet kuthibitisha kuwa sio yeye aliyedaiwa kuokolewa.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni siku 11 zimepita toka kutokee kwa tetemeko hilo lililoathiri Uturuki na Syria, Atsu amefariki akiwa na umri wa miaka 31 na amewahi kuvichezea vilabu vya Chelsea, Evertona na Newcastle.