June 16 kamati ya bunge la maadili limetangaza kuwasimamisha wabunge wawili wa viti maalum CHADEMA Susan Lymo na Anatropia Theonest kwa makosa ya kulidanganya bunge.
Mbunge Susan Lymo amehukumiwa kwa kusema jeshi la Polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha ikiwa kwamba hiyo ni idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kamati imemsimamisha vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.
Pia mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
MAMBO MANNE YA MBUNGE ROSE TWEVE ‘WATU 398 WANAFARIKI KWA KUJIFUNGUA’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE