Chui wa kike wa Malaysia mwenye umri wa miaka minne katika bustani ya wanyama nchini Marekani amepimwa na kukutwa ana na Virusi vya Corona.
Taarifa kutoka kwa Wamiliki wa bustani hiyo ya Bronx katika Mji wa New York, inasema kwamba matokeo hayo yalithibitishwa na maabara ya huduma ya afya ya mifugo Mjini Lowa.
”Nadia na dadake Azul pamoja na chui wengine wawili na simba watano wa Afrika walianza kikohozi kikavu na wote wanatarajiwa kupona kabisa,” ilisema taarifa ya uongozi wa bustani hiyo.
Chui hao wanaaminika kuambukizwa na mfanyakazi mmoja wa bustani hiyo, ”Tulimpima chui huyo kwa jina Nadia katika harakati za kuchukua tahadhari na tutahakikisha kwamba maarifa yoyote tutakayopata kuhusu Covid-19 tutayasambaza ulimwengu unaojaribu kuelewa ugonjwa huu”, alisema msimamizi wa bustani hiyo ya wanayama katika taarifa yake siku ya Jumapili.
Bustani hiyo imesema kwamba haijui virusi hivyo vitawaathiri vipi wanyama kama chui na simba kwa kuwa spishi tofauti zinaweza kuathirika tofauti kwa maambukizi mapya, lakini wanyama wote watawekwa chini ya uangalizi wa karibu.
Via: CNN
WAZURURAJI DSM KUKAMATWA “BAKI NYUMBANI, HATUTAKI KUTUMIA NGUVU”