Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kimeandaa mashindano yatakayohusisha wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi lengo la mashindano hayo ni kuwaweka Pamoja wananchi na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na uhalifu hapa nchini.
Mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa amesema mashindano hayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu na yatahusisha michezo yote ambayo washiriki wake ni maofisa wanafunzi na wakaguzi wa saidizi wa Jeshi la Polisi kutoka katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam.
Ameongeza kuwa tayari maandalizi yamekwisha kamilika kwa asilimia mia hivyo amewakaribisha wananchi wa maeneo ya karibu na chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kufika kushuhudia mashindano hayo katika chuo hicho kilichopo wilaya ya Temeke maeneo ya kurasini jijini Dar es salaam.