Katika utekelazaji wa mradi wa China Fund In Trust (CFIT) kupita Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimesaini hati ya makubaliano na Halmashauri ya Mji Mafinga na na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, hati hiyo Pamoja na mambo mengine imelenga kuwapa wanafunzi na wahadhiri wa MUST fursa katika kuwajengea uwezo na umahili, kwa kupata nafasi za mafunzo ya vitendo viwandani, kufanya tafiti, bunifu na ushauri elekezi katika Nyanja za mitambo, umeme, kilimo na ufugaji, biashara na mafunzo wezeshi kwa wahitimu ili waweze kukiajiri.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, lililofanyika katika Mji wa Mafinga Prof. Aloys Mvuma Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinoljia Mbeya, amezishukuru halmashauri hizo na kuahidi ushirikiano hasa katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na wahadhiri watakaonufaika na nafasi hizi, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika taaluma zao kwa vitendo, pia kuwajengea uwezo wahitimu wa kujiajiri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mji Mafinga Nd. Ayubu Kambi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mufindi Nd. Charles Fussi wameishukuru MUST kwa wazo hili na kuwataka wanafunzi na wahadiri kutumia vyema nafasi hiyo, ili kukuza taaluma zao.
Mradi wa CFIT Pamoja na mambo mengine unalenga kuboresha uwezo wa chuo kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na kuwawezesha wahitimu kuwa wabunifu na kuweze kujiari wenyewe na kutengeza ajira kwa wengine.
Nae Prof. Zacharia Katambara mratibu wa mradi wa CFIT, MUST anaishukuru UNESCO kwa kuleta mradi huu.