Mtu wangu wa nguvu bado mitandao inakupa nafasi ya kusafiri kifikra na kimawazo kama hujafika sehemu unaweza ukapata nafasi ya kuijua sehemu kabla hata ya kufika, February 7 nimekutana na list ya miji mitano hatari zaidi duniani stori kutoka www.cheatsheet.com , Afrika upo mji mmoja mtu wangu.
1- San Pedro Sula, Honduras
Huu ndio mji hatari zaidi duniani unatajwa kuwa na matukio kadhaa ya kiharifu, San Pedro unatajwa kuongoza kuwa na vitendo vya kiharifu kama uuzaji wa madawa, vikundi vya kihuni na umekithiri umasikini.
2- Rio de Janeiro, Brazil
Usidanganyike kwa kusikia kuwa michuano ya Kombe la Dunia na Olympic iliwahi kufanyika huko, Rio de Janeiro ni moja kati ya mji hatari zaidi duniani, licha ya kuwa unatajwa kuvutia baadhi ya matukio makubwa kufanyika.
3- Cape Town, South Africa
Ni moja kati ya miji inayovutia watalii katika nchi hiy, lakini vitendo vya kiharifu vimekubwa vikiingia kwenye headlines mara kadhaa, Cape Town sio suala geni kuona kuona vipo vikundi maalum vya vijana vipo kwa ajili ya kufanya vitendo vya kiharifu.
4- San Salvador, El Salvador
Huu ni mji kabisa ambao una vikundi vya kiharifu maarufu kama vile vipo rasmi au kutambulika kisheria, kuna vikundi vingi na maarufu vya kiharifu San Salvador kama vile MS-13, kutokana vitendo vya kiharifu kumekuwepo na watu wengi kukimbilia kaskazini mwa nchi hiyo.
5- Kabul, Afghanistan
Kabul kutokana na hali ya usalama kuwa ndogo sidhani kama kuna mtu au mtalii anaweza kuvutwa kwenda kutembea, mji huo bado unatajwa kutokuwa na hali ya amani kutona na uwepo wa wanamgambo wa Taliban na majeshi ya U.S.A.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.