Jumamosi ya December 5 Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena kwa michezo nane kupigwa, mchezo wa kwanza kupigwa ulikuwa ni mchezo kati ya Stoke City dhidi ya Manchester City katika dimba la Britannia lenye uwezo wa kuchukua mashabiki 28383. Huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwa Man City ambao wanamipango ya kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi.
Man City ambao walikuwa na point 29 kabla ya mchezo huu kuchezwa, walianza kwa kuruhusu kufungwa magoli mawili ya haraka, kitendo ambacho kilifanya mchezo kuzidi kuwa mgumu kwa Man City, kwani baada ya Stoke City kuongoza kwa goli 2-0 hadi dakika ya 80 walianza kuwa makini na ulinzi wa magoli yao hili yasirudishwe na Man City.
Mchezo ulimalizika kwa Man City ambao wapo kileleni mwa Ligi Kuu kwa muda. kwani uwezekano wa wao kuendelea kusalia kileleni kunategemea matokeo ya mechi za Leicester City, Man United na Arsenal. Mchezo wa Man City na Stoke City ulimalizika kwa Stoke kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na Marko Arnautovic dakika ya 7 na 15.
Video ya magoli ya Stoke City Vs Man City
https://youtu.be/iTt977bs4wg
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.