Kuna watu maarufu hawapendi kubadilisha nguo, Rais Obama yumo.. Kuna sababu?
Share
2 Min Read
U.S. President Barack Obama laughs at the White House Correspondents Association annual dinner in Washington April 28, 2012. REUTERS/Larry Downing (UNITED STATES - Tags: POLITICS ENTERTAINMENT MEDIA) ORG XMIT: WAS335
SHARE
Unaweza kumuona Rais Barack Obama kwenye suti moja au ya aina moja kila wakati, hapendi kubadilisha?
Marehemu Boss wa Apple Inc, Steve Jobs nae yumo kwenye list… ana sababu yoyote?
Mwingine ni jamaa Boss wa Facebook, Mark Zuckerberg… kila ukimuona ni kama anakuwa na T-shirt moja tu, unakumbuka alichokijibu alipoulizwa?
Leo nimepata sentensi zao wote watatu.
Mwaka 2012 Rais Barack Obama aliwahi kujibu sababu iliyomfanya mara nyingi aonekane kwenye suti za rangi na aina moja >> “Sipendi kuamua kuhusu nini nitakula au nini nitavaa… nina mambo mengi zaidi ya kuyafanyia maamuzi kuliko hayo“>>>Marehemu Steve Jobs.. Huyu ni mmoja wa waanzilishi wa Kampuni ya Apple Incya Marekani, yeye pia kwenye mavazi yake mara nyingi alionekana na masweta ya rangi nyeusi. Sababu yake pia kuonekana hivyo inatajwa kuwa ni ileile ya uvivu wa kufanya maamuzi mapya ya nguo ya kuvaa kila wakati.Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook nae anaonekana mara nyingi na T-Shirt ya Rangi ya kijivu, ndio anayoipendelea zaidi na alipoulizwa alijibu >>> “Natakiwa nifanye maamuzi machache na ya msingi zaidi kwa ajili ya maisha yangu na kuisaidia jamii yangu“>>> maana yake ni kwamba kwenye maamuzi yake, ishu ya kubadilisha nguo haipo kwenye hesabu zake kabisa, Mark aliwahi kusema kwamba sio kwamba habadilishi nguo ila anazo T-shirt nyingi za kijivu na ndio alizoamua kuzivaa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,TWITTER,FB, YOUTUBE