Wakati kukiwa na sintofahamu juu ya kumalizika au kutomalizika kwa misimu ya soka katika nchi mbalimbali duniani, vilabu 20 Italia vimependekeza kumaliza msimu.
Vilabu hivyo vimepiga kura msimu uendelee kama kawaida na usikatishwe, hivyo hadi sasa ni wazi Italia watatafuta namna ya kumalizia msimu wa Ligi.
Nchini Italia club zinaripotiwa kuwa zinaweza kuanza mazoezi May 18 baada ya kumalizika kwa Lockdown May 17, Italia ni miongoni mwa nchi za Ulaya zilizoathirika na corona kwa kiasi kikubwa.