Chama cha Waongoza Watalii Tanzania kimetembelea eneo ilikotokea ajali ya Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent na kuzungumzia ishu muhimu wanazotamani zifanyiwe kazi mapema.
“Tumekuja mahali hapa ili kuwakumbuka wale watoto wetu Wapendwa ambao walipoteza maisha yao katika eneo hili, sisi kama Waongoza Watalii tumeguswa kwa namna nyingi na katika wale waliofariki ni mtoto wa mmoja wetu”
“Hatujapatendea haki mahali hapa, naomba Viongozi wa Wilaya ya Karatu wawashirikishe Wadau wengine kama vile hifadhi ya Manyara, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Wadau wenye Mahoteli kwenye eneo hili la Karatu ili tuwaenzi Watoto waliopoteza maisha eneo hili, tujenge mnara ambao utakua kumbukumbu, tukio lile ni kubwa na limetengeneza historia kwenye nchi yetu”
Haya yote yamesemwa na Chama cha Waongoza Watalii Tanzania ambao walifika kwenye eneo hilo na kufanya usafi ikiwa ni kampeni yao ya kuhakikisha usafi unakua jambo la kwanza, unaweza kutazama kwenye hii video hapa chini