Kwa muda mrefu sana ligi kuu ya England imetawaliwa na makocha ambao asili yao halisi si nchi hiyo bali nje ya taifa hilo.
Makocha waliotawala ligi ya England kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakitoka nje na hasa kwenye taifa la Scotland ambalo limetoa makocha mahiri na wenye historia kama Bill Shankley, Bob Paisley, Matt Busby, Sir Alex Fergusson na wengine.
Makocha wa Scotland wamekuwa na historia kubwa kwenye ligi ya England lakini historia hii inaonekana kukaribia kuisha hasa kutokana na matukio ya hivi karibuni katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Kufukuzwa kazi kwa kocha wa Aston Villa, Paul Lambert kumemaanisha kuwa hivi tunavyozungumza ligi ya England haina kocha mkuu ambaye ni raia wa Scotland kati ya timu zake 20 zinazoshiriki ligi hiyo.
Ilikuwa imezoeleka kuona makocha wa Kiskochi wakitoa upinzani kwneye ligi hasa miaka minne iliyopita ambapo makocha kama Sir Alex Fergusson, David Moyes, Alex McLeish na Steve Kean wakifanya yao nchini England.
Muda si mrefu idadi yao iliongezeka baada ya kuja kina Paul Lambert ambaye alikuja na Norwich City pamoja na Malcky Mackay ambaye alikuja na Cardiff City.
Bada ya hapo makocha hawa walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine wakiondoka kwa sababu tofauti kuanzia kufukuzwa kazi mpaka kustaafu kwa sir alex ferguson .
Leo hii kuondoka kwa Paul Lambert kumeitia ligi ya England katika umasikini wa makocha raia wa Scotland ambao wamezoeleka kwa uhodari wao wa kujenga timu bora ambazo zimejengwa kwa misingi ya ushirikiano na ujasiri wa wachezaji na Imani kubwa ya kushinda kwa mbinu yoyote ile itumikayo mchezoni .
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook