Kampuni ya Coca-Cola imekuwa miongoni mwa wadhamini wakuu katika Tamasha la kimataifa la vyakula maarufu ‘Internation Food Carnival’ lililofanyika kwa siku mbili mfululizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ambapo mamia ya watu walikusanyika kwenye viwanja vya Green Oysterbay, kusherehekea utofauti wa vyakula mbalimbali.
Tamasha hilo, lililovutia wapenzi wa vyakula, familia, na watalii, liliwaletea washiriki fursa ya kufurahia aina mbalimbali za vyakula vya ndani na nje ya nchi, likitoa jukwaa muhimu la kubadilishana tamaduni. Kampuni ya Coca-Cola ilikuwa ni sehemu ya Tamasha hili ambapo vinywaji vyake maarufu vilitumika sambamba na vyakula hivyo, ikiwemo vyakula vya kitanzania pamoja na ladha za kimataifa na kukamilisha mlo kamili kwa washiriki mbalimbali.
“Tulilenga kuandaa tukio ambalo watu wanaweza kufurahia chakula kitamu kutoka sehemu mbalimbali duniani, lakini pia kuonja furaha ya kuwa pamoja,” alisema Moureen Ian, Mwandaji wa Tukio la Tamasha la Chakula la Kimataifa. “Ushiriki wa Coca-Cola umefanya wahudhuriaji wetu wafurahie zaidi kwani wanaweza kuchanganya vyakula na vinywaji mbalimbali kutoka Coca-Cola.”
Tamasha hilo lilikuwa na michezo mbalimbali ya kuburudisha, vibanda vya picha, na zawadi mbalimbali. Washiriki walipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, jambo lililoongeza msisimko zaidi kwa wahudhuriaji.
Ushiriki wa Coca-Cola katika tamasha hili umelenga kuimarisha uhusiano na jamii na kudumisha tamaduni, huku ikiunda kumbukumbu za kipekee kwa washiriki. Uwepo wa chapa hiyo katika Tamasha la kimataifa la vyakula la 2024 umesaidia kuboresha hali ya tukio hilo, na kufanikisha kuwa miongoni mwa matukio ya kukumbukwa jijini Dar es Salaam.