Mahakama ya Juu ya Comoro Alhamisi iliidhinisha mipango ya Rais aliye madarakani Azali Assoumani kuwania muhula mwingine katika uchaguzi ujao unaotarajiwa tarehe 14 Januari.
Assoumani atakuwa anawania muhula wa nne, baada ya kushinda uchaguzi wake wa tatu mwaka 2019.
Atakabiliana na wapinzani tisa, kulingana na orodha ya wagombea walioidhinishwa na Mahakama ya Juu.
Hawa ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani na Salim Issa, daktari na mshika bendera wa Juwa, chama cha rais wa zamani Ahmed Abdallah Sambi ambaye mwaka 2022 alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa “uhaini mkubwa.”
Uchaguzi huo unakabiliwa na uwezekano wa kususiwa na wapinzani ambao wanasema mchakato wa uchaguzi hauna uwazi na watashiriki tu ikiwa masharti fulani, kama vile kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa yatatimizwa.
Taifa hilo dogo la visiwa lililo katika Bahari ya Hindi lina wakazi 800,000 tu. Imeshuhudia mapinduzi zaidi ya 20 au majaribio ya mapinduzi tangu uhuru kutoka kwa Ufaransa katika miaka ya 1970.
Assoumani, afisa wa zamani wa jeshi, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka wa 1999