Ni siku moja baada ya uongozi wa Chelsea ya Uingereza kutangaza kumpa mkataba wa miaka mitatu kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ambaye atajiunga na klabu yao mwishoni mwa msimu. Leo April 5 Antonio Conte ameripotiwa kuwa, huenda akafungwa miezi sita.
Muendesha mashtaka Roberto Di Martino kutoka Italia anaripotiwa na Sky Sports kuwa April 5 2016 ameendeleza shauri la Conte kutuhumiwa kwa upangaji wa matokeo ya mechi ya ushindi wa Siena wa goli 1-0 dhidi ya Albinoleffe May 2011 na sare ya goli 2-2 dhidi ya Novara May 2011.
Kama Antonio Conte atakutwa na hatia huenda akakutana na kifungo cha miezi sita, Conte alituhumiwa kujihusisha na upangaji wa matokeo msimu wa 2010-2011 wakati akiwa kocha wa klabu ya Siena ya Italia.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
KAMA ULIKOSA KUTAZAMA VIDEO YA MAGOLI YA YANGA VS KAGERA SUGAR, FULL TIME 3-1