Mashindano ya mwakani ya Copa America nchini Marekani yataanza kutimua vumbi Juni 20, na fainali kuchezwa Julai 14.
Shirikisho la kandanda la Amerika Kusini CONMEBOL lilithibitisha tarehe hizo Jumanne lakini lilisema waandalizi wa mashindano bado hawajachagua miji waandaji.
Timu kumi za Amerika Kusini pamoja na sita kutoka Amerika ya Kati na Kaskazini zitashiriki katika Copa America ya 2024. Argentina ndiye bingwa mtetezi. Michuano ya awali ya Copa America iliyofanyika Marekani mwaka 2016 pia ilijumuisha timu 16.
Rais wa CONMEBOL Alejandro Dominguez alisema katika taarifa yake kwamba “toleo jipya litawaalika (mashabiki) kusherehekea na kuishi shauku ambayo shindano hili linatufanya tujisikie”.
Muundo huo, uliotangazwa hapo awali, utajumuisha timu sita za Concacaf zitakazofuzu kupitia mashindano ya Ligi ya Mataifa ya 2023-24.
Kwa timu za kitaifa za wanawake, Concacaf imealika timu nne bora za kitaifa za CONMEBOL kushiriki Kombe la Dhahabu la Concacaf W 2024. Toleo la uzinduzi wa dimba hili la timu 12 pia litachezwa nchini Marekani.
Timu mbili za Concacaf zitakazoshiriki Olimpiki ya Majira ya 2024 (Marekani na Jamaica au Kanada) zitafuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dhahabu la Concacaf W 2024. Timu sita zilizosalia za Concacaf zitaamuliwa kupitia 2023 Road to Concacaf W Gold Cup.
Timu nne za wageni za CONMEBOL zitakazoshiriki zimeamuliwa kulingana na matokeo ya Copa America ya Wanawake 2022: Brazil (bingwa) Colombia (mshindi wa pili), Argentina (nafasi ya tatu) na Paraguay (nafasi ya nne).
Copa América hushirikisha timu zote za kitaifa za Amerika Kusini, ikiwa ni pamoja na Brazil na Argentina, lakini pia kihistoria zimealika nchi zilizoalikwa kushiriki.