Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameagiza Ofisi zote za umma Mkoani humo kununua mitambo maalumu ambayo imebuniwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must) ambao unawawezesha wananchi kunawa mikono bila kugusa kitu chochote kama sehemu ya kukabiliana na maradhi ya Corona.
Chalamila ametoa agizo hilo wakati alipokuwa anapokea moja ya mitambo hiyo ambao utakuwa unatumika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo amesema Ofisi zote zinatakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku 15.
Aidha ameuagiza uongozi wa Chuo hicho kutengeneza mitambo mingi na kuipeleka bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya wabunge kuinunua na mingine ipelekwe Ikulu ya Chamwino.