Katika juhudi za kukabiliana na corona Rwanda imezindua mashine ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo ambayo inawasaidia wagonjwa kupumua (Ventilator).
Ni mashine iliyotengenezwa na vijana wanane wa chuo kikuu cha Rwanda kwa msaada wa wakufunzi wao na lengo likiwa ni kuitua serikali mzigo wa kuagiza mashine kama hizi kutoka nje.
Kwa kawaida mashine hii inayomsaidia mgonjwa aliyeko mahututi kupumua wenyewe wanasema thamani yake ni USD Elfu 10 (wastani wa Tsh. Million 23) inaponunuliwa kutoka Nchi za nje.
Hata hivyo mabingwa walioitengeneza wanasema kwamba kwa sasa kutokana na Dunia kukabiliwa na tatizo la corona bei ya mashine hii imepanda hadi USD Elfu 20 (wastani wa Tsh. Million 46)
Source Kutoka Idhaa ya Kiswahili