Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Qu Dongyu, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Roberto Azevedo, wameonya leo juu ya uhaba mkubwa wa chakula unaoelekea kuikumba Dunia, iwapo serikali zitashindwa kusimamia vizuri janga la corona.
Serikali nyingi kote Duniani zimetoa amri ya Raia wake kubaki majumbani na kusababisha kupungua kwa kasi ya biashara ya kimataifa na usambazaji chakula.
Watu wananunua bidhaa kwa wingi kutokana na hofu na kuonesha tayari kuzidiwa kwa hatua za usambazaji chakula huku maduka ya kujihudumia yakibaki bila bidhaa katika Mataifa mengi.
Taarifa ya pamoja iliyotiwa saini na Viongozi hao, imesema kutokuwa na uhakika wa kupatikana kwa chakula huenda kukachochea wimbi la vikwazo vya kuuza chakula nje na kusababisha majanga kwenye soko la Kimataifa.
WAFANYAKAZI TBC WASHINDWA KUJIZUIA, VILIO VYATAWALA MWILI WA MARIN HASSAN UKIAGWA