Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Dorothy Gwajima leo July 23,2021 amesema Tanzania tuna vifo 29 vya Ugonjwa wa Corona huku waliolazwa 176 kwa siku moja.
‘Tatizo la Corona lipo na linagharimu Watu uchumi na uhai, jana nilitangaza kuwa July 21,2021 tulikuwa na wagonjwa waliolazwa 682 Nchi nzima (ambao ndiyo tuliweza kuzifikia takwimu zao) kwa jana peke yake wagonjwa wapya waliolazwa kwa takwimu zilizotufikia walikuwa 176, ikumbukwe hawa ndio walioripoti vituo vya huduma za afya na huenda wengine wako majumbani”
“Vilevile, ikumbukwe kwamba sio kwamba Watu hawafariki la hasha wanafariki na kwa takwimu za July 21, 2021 waliofariki ni 29 kwa takwimu zilizotufikia, itoshe kusema tatizo lipo, lazima tusimame tupambane bila kuathiri shughuli zetu za uchumi na kutiana hofu tukajikuta tumeongezea tatizo lingine”———Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Dorothy Gwajima akiwa Dar es salaam leo
“Tatizo la Corona lipo na linagharimu Watu uchumi na uhai, jana nilitangaza July 21,2021 tulikuwa na wagonjwa waliolazwa 682 Nchi nzima, kwa jana peke yake wagonjwa wapya waliolazwa walikuwa 176, kwa takwimu za July 21,2021 waliofariki ni 29”——Waziri Gwajima