Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa kwa sasa imepata mashine mpya na za kisasa zenye uwezo wa kutoa vitambulisho 9000 kwa siku.
Hayo yamebainishwa na Msemaji wa NIDA, Geofrey Tengeneza, ambapo amesema kuwa zoezi la utoaji wa vitambulisho limeathiriwa na janga la Virusi vya Corona, ambapo kwa sasa wananchi wengi hawajitokezi ofisini hapo kwa kuogopa kupata maambukizi.
Aidha NIDA imetoa wito kwa wananchi ambao hawajapata vitambulisho, wajitokeze ili waweze kupatiwa kwa kuwa ni muhimu na si tu kwa ajili ya kusajili laini za simu.