Mara nyingi watu huwa wanalalamika, wanasema viongozi na watu wenye pesa hata wakifanya makosa hawafungwi, lakini ikitokea mtu wa kawaida kafanya kosa lolote anahukumiwa kifungo, hapo ndio ambapo watu wanalalamikia kwamba inaonekana kama hakuna usawa kwenye Sheria.
Mahakama ya Ivory Coast imemhukumu Simone Gbagbo mke wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo kifungo cha miaka 20 gerezani.
Simone amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu tatu.
Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, Laurent Gbagbo ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu ICC iliyopo The Hague, Uholanzi kwa makosa hayo kutokana na machafuko yaliyotokea mwaka 2010 baada ya Rais huyo kugoma kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara aliyeshinda nafasi ya Urais kutoka chama cha upinzani.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook