Kamishna wa Operesheni na mafunzo CP Awadhi Juma Haji amefunga mafunzo ya mbinu za medani za kivita kwa kundi la maafisa na wakaguzi wasaidizi wa Polisi wanafunzi yaliyoanza oktoba 20, Mwaka huu katika kambi ya Jeshi la Polisi iliyopo Kijiji cha mkundi mbaru Mkomazi wilaya ya korogwe Mkoani Tanga.
Akifunga mafunzo hayo kamishna Awadhi ametuma salam kwa watu wenye nia ya kufanya uhalifu kuwa Jeshi hilo liko imara ambapo amebainisha kuwa alitomuonea muhali mtu yoyote atakaye chezea amani ya nchi.
CP Awadhi ameongeza kuwa Mkuu wa Jeshi hilo IGP camillus Wambura kwa sasa amewekeza katika mafunzo kwa maafisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika vyuo vya ndani ya nchi na nje ya nchi lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi wa kisasa na unaoendena na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa Jeshi la Polisi nchini.
Pia amemshukuru Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameliwezesha Jeshi hilo kwa kulipatia bajeti iliyowezesha mafunzo kwa maafisa,wakaguzi ma askari wav yeo mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt Lazaro Mambosasa amemshukuru Kamishna wa Operesheni na mafunzo kwa namna ambavyo kamisheni hiyo imekuwa ikisimamia mafunzo hayo ya maafisa na wakaguzi wasaidizi wa Polisi wanafunzi.