Leo January 8, 2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkoa wa Arusha imevifunga vituo vinne vya mafuta kwa kosa la kukwepa kodi na kushindwa kutoa risiti za eletroniki (EFDs) za mauzo wanapouza mafuta ambapo imewatoza faini ya Shilingi Milioni 580 wafanyabiashara 129.
Meneja wa TRA mkoa wa Arusha, Faustine Mdesa amesema kwamba kufungiwa kwa vituo hivyo vya mafuta kumetokana na wafanyabiashara hao kutotii agizo la serikali la kufunga mfumo wa risiti za EFDs kwenye pampu za mafuta.
Ameeleza kuwa wafanyabiashara wanaokamatwa kwa kutotoa risiti wamekuwa wakitozwa faini ya shilingi milioni 4.5 na wale ambao wananunua bidhaa bila kuchukua risiti hutozwa shilingi milioni 1.5.
Fedha zilizokusanywa na TRA kwa nusu ya Mwaka wa Fedha 2017/18
BREAKING: Msemaji Mkuu wa Serikali anazungumza na waandishi