Ukarimu wa CRDB BANK haujaanza leo….. ni siku nyingi tumekua tukiona jinsi wanavyogusa watu huku mtaani ambapo leo ni zamu ya Mwanamke mwenye watoto nane Temeke Dar es salaam ambaye alishakata tamaa hajui atakimbilia wapi baada ya mume wake kufariki.
Ni kisa kilichogusa wengi sana, yani alikua na watoto wanne tayari alafu akapata ujauzito na kujifungua Watoto wanne kwa mkupuo hivyo idadi ya watoto wake wote ikawa ni 8 lakini akiwa na ujauzito wa miezi mitatu alifiwa na Mume wake.
Ugumu ulikuja kwasababu Mume wake amefariki miezi sita kabla hajajifungua hao Watoto wanne na hakujua atakimbilia wapi au atawezaje kuwasaidia lakini Bank ya CRDB tawi la Temeke baada ya kusikia taarifa hizo ikafanya spidispidi ili kumsaidia huyu mama.
Meneja wa CRDB Temeke Diana Mtalo ndio alisimamia hili zoezi mwanzo mwisho ambapo kwa maagizo yake pia, ametoa order ambayo itatekelezwa kila mwezi ambapo Mama huyu atakua akiwekewa pesa kila kwenye account yake aliyofunguliwa CRDB Temeke.
Jingine aliloliagiza Diana baada ya kukutana na familia hii siku ya mtoto wa Afrika na kufuturu pamoja ni Watoto wote hao kufunguliwa Account CRDB Temeke, kununuliwa chakula cha kutosha kuwasaidia nyumbani pamoja na nguo na vitu vyote vya malezi ya watoto hao waliozaliwa yani kwa ufupi ni kwamba hawatopata shida tena.